First Aid training page
Did you know that there are great benefits that you will get by undergoing First Aid Training with St John?
People who are trained in First Aid are usually more responsible and safety-conscious, thereby reducing the level, frequency and cost of accidents and injuries. If accidents do occur, having someone who has been trained in First Aid can make the vital difference ...they can save a life. First Aid is a valuable skill that all of us MUST have.
The laws of Tanzania (Occupational Health and Safety Act 2003 – Section 58, Para 1 & 2) require that in every place of work, be it an office, factory, plantation, supermarket or learning institution, that there is a person trained in First Aid by a recognised institution as well as a clearly marked First Aid box.
St John is therefore here to help you! We are a recognised provider of First Aid and part of a global organisation which specialises in training First Aid.
St John Ambulance Tanzania offers the Lifesaver International First Aid Course (LIFAC) which covers:
- Basic Emergency care
- Accident care
- Medical Emergency care
- Emergency Childbirth
- Additional information: (Common Infectious diseases, HIV and AIDS awareness)
Each participant receives a comprehensive First Aid book as part of the course fee.
Why chose St John?
- We have highly qualified, experienced trainers
- We use state of the art training equipment
- We provide internationally recognised certificates to those students who pass.
We can offer the training at our newly renovated training room at the Dar es Salaam Trade Fair Ground, or we can come to you!
For more information on the course and the course costs, please email Alliy Lyeme the Secretary General St John Ambulance on stjohnassotz@yahoo.com or Telephone No. +255222850834
Ukurasa wa Mafunzo ya Huduma ya Kwanza
Unajua kwamba kuna manufaa makubwa ambayo utayapata ukifundishwa Huduma ya kwanza na St John?
Watu ambao wanafundishwa Huduma ya Kwanza mara nyingi wanakuwa wanawajibika na wenye usalama, hivyo kupunguza kiwango, gharama, na kupunguza kufululiza kwa ajali na majeraha.
Ikiwa ajali itatokea, na kuna mtu ambaye amefundisha Huduma ya Kwanza kutakuwa na tofauti kubwa kuliko ikiwa hakuna mwenye ujuzi huo… wanaweza kuokoa maisha. Huduma ya Kwanza ni ujuzi wa thamani ambao kila mmoja wetu LAZIMA awe nao.
Sheria yetu ya Tanzania kuhusu afya na usalama wa viwandani ya mwaka 2003- sehemu ya 58 kifungu cha 1 na 2 (Occupational Health and Safety Act 2003 – Section 58, Para 1 & 2) inaagiza kuwa lazima awepo mtu aliyefundishwa Huduma ya Kwanza na chombo kinachotambulika na kuwa na sanduku la Huduma ya Kwanza ambalo limewekewa alama zilizo wazi mahali pa kazi, iwe ni ofisini, kiwandani, kwenye mradi, duka la vifaa vya aina mbali au mashule na vyuoni.
St John ipo hapa kukusaidia! Sisi tunatoa Huduma ya Kwanza kwa kiwango cha kimataifa na sisi ni sehemu ya mtandao mkubwa duniani ambao tumebobea katika kufundisha na kutoa Huduma ya Kwanza.
St John Ambulance Tanzania inafundisha Huduma ya Kwanza ya kimataifa ya kuokoa masiha ambayo inakuwa na mafunzo yafuatayo:-
- Mambo muhimu ya kwanza wakati wa dharura
- Jinsi ya hudumu katika dharura
- Matibabu wakati wa dharura
Kumsaidia mama wakati wa uzazi wa dharura - Magonjwa ya kuambukiza: (Kutoa elimu juu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi, Na mambo mengi mengineyo)
Kila mshiriki kwa kutumia gharama za mafunzo anapata kitabu cha Huduma ya Kwanza kama sehemu ya mafunzo yake.
Kwa nini uchague St. John?
- Tunao wakufunzi ambao wamehitimu na wana ujuzi wa muda mrefu wa kufundisha.
- Tunatumia vifaa vya kisasa katika kufundisha.
- Tunatoa vyeti vinavyotambulika kimataifa kwa wanafunzi wetu ambao watafaulu.
Kwa sasa tunatoa mafunzo haya katika kituo chetu kipya cha mafunzo ambacho kipo Dar Es Salaam katika uwanja wa Saba saba au tunaweza kukufikia mahali ulipo!!
Kwa ajili ya taarifa zaidi kuhusu mafunzo na gharama zake, tafadhali usisite kutuma barua pepe stjohnassotz@yahoo.com au simu nambari +255222850834 kwa Ndugu Alliy Lyeme Katibu Mkuu wa St John Ambulance Tanzania.
